Maukibu ya kuomboleza imehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Afdhalu Shami, baadhi ya viongozi na watumishi wa mawakibu na kundi kubwa la waombolezaji.
Amesema “Watu wa Karbala wamezowea kuomboleza kifo cha mbora wa wanawake wa duniani (a.s) kwa kumpa pole kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s) mbele ya kaburi lake tukufu katika mji wa Najafu”.
Akaongeza kuwa “Maukibu ya kuimboleza ni utamaduni wa watu wa Karbala kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ambazo zimetoa mahitaji yote ya kuomboleza kifo cha Bibi Zaharaa (a.s)”.
Akabainisha kuwa “Maukibu inahusisha mawakibu nyingi na vikundi vya Husseiniyya katika mkoa wa Karbala pamoja na waombolezaji kutoka mkoa huo”.


















