Atabatu Abbasiyya inatembelea familia za mashahidi na majeruhi wa Lebanon nchini Siria.

Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya umetembelea familia za mashahidi na majeruhi wa Lebanon zilizokimbilia Siria, kwa lengo la kujua mahitaji yao.

Rais wa ujumbe huo nchini Siria Sayyid Khaliil Hanuun amesema “Tumetembelea familia za mashahidi na majeruhi wa Lebanon zilizopo Siria, ili kutambua mahitaji yao na kuangalia namna ya kuwasaidia, ikiwa ni sehemu ya kushikamana na ndugu zetu raia wa Lebanon katika wakati huu ambao wanashambuliwa na mazayuni”.

Akaongeza kuwa, ziara yetu imehusisha utoaji wa bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) na zawadi zingine, yote ikiwa ni sehemu ya juhudi za Atabatu Abbasiyya za kusaidia wakimbizi wa Lebanon waliopo Siria, na kuitikia wito wa Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu”.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeshatuma misafara sita yenye maelfu ya tani za misaada kwa wakimbizi wa Lebanon waliopo Siria, sambamba na kujenga hospitali, kutuma kikosi cha madaktari bingwa, shehena za dawa na chakula kwa ajili ya kusaidia familia za walebanon, aidha tumeandaa jiko kubwa kwa ajili ya kupika chakula na kugawa kwenye vituo vya wakimbizi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: