Kitengo cha maarifa kimetoa chapisho la ishirini na saba la jarida la (Raddu-shamsi)

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimechapisha toleo la ishirini na saba la jarida la (Raddu-shamsi).

Uchapishaji wa jarida hilo unasimamiwa na kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo.

Madhumuni ya chapisho hilo yanaendana na turathi za Hilla, linampa msomaji picha ya mji wa Hilla katika karne zilizopita upande wa Fiqhi, Adabu na historia.

Jarida limeandika mambo mbalimbali kuhusu turathi za mji wa Hilla na wanachuoni wake, wahadhiri na shule za kidini, sambamba na kuandika sekta ya maisha ya kijamii na kiuchumi katika mji huo, ikiwemo Makala kuhusu (Sayyid Ali Hadidi) kupitia mlango wa malalo, Makala nyingine inahusu (Hazina ya vitabu vya kielimu katika mji wa Hilla), maudhui yenye anuani isemayo (Hilla katika nyaraka za kitaisha na kimataifa).

Nalo ni miongoni mwa majarida muhimu katika mji wa Hilla, hupokea michango ya waandishi, watafiti, waimbaji wa qaswida, mashairi na wapigapicha wa turathi za mji wa Hilla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: