Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika kuhuisha siku za Fatwimiyya kwenye chuo kikuu cha Kufa.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika kuhuisha siku za Fatwimiyya kwenye chuo kikuu cha Kufa.

Hafla imefanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Urithi wa kiroho wa Fatuma Zaharaa –a.s-) kwa kushirikiana na kitivo cha mipango ya majengo katika chuo.

Kiongozi wa Maahadi Bibi Manaar Aljaburi amesema “Maahadi imeandaa hafla ya usomaji wa Qur’ani katika kitivo cha mipango ya majengo, inavipengele vingi, usomaji wa Qur’ani kwa sauti ya mwanafunzi Fatuma Hassan, usomaji wa qaswida inayo muelezea Bibi Zaharaa (a.s) kutoka kwa kiongozi wa idara ya habari katika Maahadi Dokta Israaa Akarawi”.

Akaongeza kuwa “Vipengele vya hafla ya usomaji wa Qur’ani vimehusisha usomaji wa qaswida na mashairi kutoka kikundi cha Nab’ul-Juud zenye anuani isemayo (Safari ya kujitolea) zimepata muitikio mkubwa kutoka kwa wahudhuriaji”.

Akabainisha kuwa “Maahadi hufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani, kwa lengo la kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani tukufu na kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: