Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya matengenezo ya gari zinazotumia umeme na mitambo mingine ya umeme.
Kiongozi wa idara ya ukarabati wa gari za kuchaji kwa umeme, Sayyid Hasanain Ali Abudi amesema “Kitengo kimefanya ukarabati wa mitambo inayotumiwa na vitengo vya Ataba, ipatayo 92 na kusafisha mitambo yote ya umeme pamoja na kuweka mitambo ya hakiba kutokana na kuingia msimu wa masika”.
Akaongeza kuwa “Matengenezo yanahusisha njia za umeme, kubadilisha betrii zilizotumika, kufunga nailoni kwa ajili ya kuzuwia zisifikiwe na maji ya mvua wakati wa kuhamishwa sehemu moja kwenda nyingine”.
Akasema kuwa “Kazi ya ukarabati ilianza mwanzoni mwa mwezi wa kumi, tumekua tukifanya matengenezo kila siku na kuhakikisha mitambo yetu ipo katika hali nzuri ya kuhudumia mazuwaru wakati wote”.






