Mji mtukufu wa Karbala, umeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru waliokuja kuhuisha usiku wa Ijumaa mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mji wa Karbala hupokea idadi kubwa ya watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhuisha utiifu wao kwa Ahlulbait (a.s).
Atabatu Abbasiyya kupitia vitengo vyake vyote, hutoa huduma tofauti kwa mazuwaru kulingana na mahitaji yao.










