Ratiba ya ufunguzi wa kongamano la Al-Ameed kimataifa awamu ya saba, imepambwa na filamu yenye anuani isemayo (Mashuke saba ya kijani) inayo onyesha mihtasari ya makongamano ya nyuma.
Uonyeshaji wa filamu ni sehemu ya ratiba ya siku ya kwanza ya kongamano la Al-Ameed kielimu na kimataifa awamu ya saba, linalosimamiwa na jumuiya ya Al-Ameed kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Alkafeel na Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, linakauli mbiu isemayo (Tunakutaka katika uwanja wa Al-Ameed kujifunza), na anuani isemayo (Amani ya familia na jamii: utambulisho wa kupambana na changamoto), litadumu siku mbili.
Filamu imeonyesha mambo makuu yaliyofanywa katika makakongamano yaliyopita, kuanzia ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, hadi katika uteuzi wa mada na maandalizi ya kongamano hili la sasa.
Kongamano hili linamada zitakazowasilishwa kwa lugha ya kiarabu na kiengereza, mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na tafiti za kijamii na kibinafsi, Amani ya familia na jamii, Dini na turathi na Amani ya fikra.



