Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Didah Mussawi amesema kuwa, Amani ya familia na jamii ni kipaombele chetu kikubwa.
Ameyasema hayo katika ratiba ya siku ya kwanza ya kongamano la Al-Ameed kielimu na kimataifa linalofanywa chini ya Ataba tukufu kwa kushirikiana na Jumuiya ya Al-Ameed pamoja na chuo kikuu cha Alkafeel na Al-Ameed, chini ya kauli mbiu isemayo (Amani ya familia na jamii: utambulisho wa kupambana na changamoto) na kauli mbiu isemayo (Tunakutana katika uwanja wa Al-Ameed kujifunza), litadumu siku mbili.
Akasema “Amani ya familia na jamii ni maudhui inayo endana na malengo ya Atabatu Abbasiyya, kwani Ataba ni taasisi ya kidini na kibinaadamu yenye lengo la kuhudumia mtu popote alipo”
Akaongeza kuwa “Familia ni msingi wa kujenga jamii, inatakiwa kupewa mafundisho ya Dini na kibinaadamu”, akasema kuwa “Misingi ya Dini imekuwa ikipigwa vita na makundi maovu yanayolenga kuharibu familia”.
Akaongea kuhusu umuhimu wa kongamano la Al-Ameed, ambalo ni mkusanyiko wa kibinaadamu kimataifa, wanashiriki watafiti kutoka nchi za kiarabu na kiajemi, wanawasilisha mada kuhusu changamoto za familia kwa ujumla.






