Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imefanya program ya (pambo la maisha) kwa watoto, chini ya Ataba tukufu.
Program imefanywa katika kituo cha Swidiqatu Twahirah (a.s), kwa lengo la kujenga uwezo wa watoto katika kuhifadhi na kuelewa Qur’ani.
Ratiba imehusisha vipengele tofauti, kikiwemo kipengele cha (sura na picha) kinacholenga kuhifadhisha watoto sura fupi kwa njia rahisi inayosaidia kuhifadhi kwa wepesi.
Idara inaendelea na ratiba ya (pambo la maisha) inayosaidia kuinua kiwango cha usomaji wa Qur’ani kwa watoto.