Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu ndani ya ukumbi wa utawala katika Ataba tukufu.
Mhadhiri wa majlisi Shekhe Ahmadi Rabii amesema “Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) ndani ya ukumbi wa utawala, kwa mujibu wa riwaya ya tatu mbele ya watumishi wa Ataba tukufu”.
Akaongeza kuwa “Muhadhara umejikita katika kueleza utukufu wa Bibi Zahara (a.s) na dhulma aliyofanyiwa, sambamba na kusoma qaswida na tenzi zinazomuhusu Bibi Zaharaa (a.s)”.
Atabatu Abbasiyya hufanya majlisi za kuomboleza kumbukumbu za vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kwa lengo la kuhuisha utajo wao na kusambaza elimu na utukufu wao.










