Mazuwaru wanaomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) mbele ya Ataba mbili takatifu

Maelfu ya mazuwaru wameomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, mbele ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala.

Barabara zinazoelekea kwenye malalo mbili tukufu katika mji wa Karbala, zimeshuhudia idadi kubwa ya watu kutoka ndani na nje ya mji, waliokuja kutoa pole kutokana na msiba huo.

Atabatu Abbasiyya imejiandaa kutoa huduma kulingana na mahitaji yao, imeimarisha ulinzi, inatoa huduma za afya, chakula, maji pamoja na huduma zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: