Kamati ya maandalizi ya kongamano la kielmimu kwa vijana imefanya kikao cha kwanza.
Kongamano hilo linasimamiwa na kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na jumuiya ya Al-Ameed tarehe 19/20-12-2024.
Mjumbe wa kamati ya maandalizi na mkuu wa kituo cha Multaqal-Qamaru Shekhe Harith Daji amesema “Kikao cha maandalizi ya kongamano la kielimu kwa vijana kimehudhuriwa na wawakilishi wa vitengo vingi vya Ataba tukufu”.
Akaongeza kuwa “Kikao kimejadili ratiba ya kongamano na mwenendo wake namna utakavyo jenga uwelewa kwa vijana”.
Akaendelea kusema “Maandalizi yote ya kiutawala yamekamilika, vitengo vyote vya Ataba tukufu vipo tayali kutoa ushirikiano wowote unaohitajika”, akasema kuwa “Kongamanono linatarajiwa kuwa na matokeo chanya ya kielimu kwa vijana”.


