Hivi karibuni kituo cha Shekhe Tusi cha masomo na utafiti, chini ya kamati kuu ya kuhuisha turathi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimechapisha kitabu cha Malkia wa Roma.
Kitabu hicho kimeandika tukio la ndoa ya Bibi Narjisi mama wa Imamu Hujjah (a.f) “Malkia wa Roma”, kimefafanua mambo tofauti ya kihistoria na kijografia”.
Muandishi wa kitabu hicho Shekhe Hassan Yusufu bun Nakhi amejibu utata uliokua unatolewa kuhusu mama wa Imamu wa zama (a.f) na jinsi alivyo olewa na Imamu Hassan Askariy (a.s) sambamba na kutaja utata unaotolewa kuhusu riwaya.
Kimethibitisha kuwa Bibi Narjisi (a.s) anatokana na nasaba ya Mfalme wa Roma kwa shuhuda za riwaya, vitabu vya hadithi, Lugha, Adabu, Historia Uislamu, historia ya Bezenti, Jografia, Joyolojia, Ukristo, Historia ya Kanisa na fani zingine nyingi zinazothibitisha utakatifu wa mama wa Imamu wa zama.