Kikao kimeongozwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini mbele ya wawakilishi wa Ataba tukufu za Iraq.
Sayyid Aalu Dhiyaau-Dini amesema “Kikao kimejikita katika kueleza umuhimu wa kudumisha mawasiliano baiana ya Ataba na kubadilishana uzowefu katika mambo mbalimbali, kama vile afya, elimu, malezi, Dini, utamaduni na mambo mengine”.
Akaongeza kuwa “Tumejadili namna ya kutoa huduma bora kwa mazuwaru”, akaeleza “Umuhimu wa kupokea mamilioni ya mazuwaru kwa mwaka”.
Kikao kimehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya bila kumsahau mwenyeji wao katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.