Majmaa-Ilmi imechapisha kitabu kuhusu Qur’ani tukufu na umuhimu wake.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imechapisha kitabu kipya chenye anuani isemayo (Qur’ani tukufu na umuhimu wake katika maisha yetu) cha mtunzi Shekhe Aamir Al’amiriy.

Kitabu kinaonyesha umuhimu wa Qur’ani tukufu katika maisha yetu ya kila siku, kwani ndio katiba ya Mwenyezi Mungu inayoratibu maisha ya mwanaadamu.

Kitabu hicho ni sehemu ya mfululizo wa vitabu vinavyoenda kwa jina la (Qutufu), vinavyo fundisha madhumuni ya Qur’ani na kumfanya msomaji aelewe kwa njia rahisi.

Kitabu kinapatikana sehemu zifuatazo:

  • 1- Barabara ya Posta ofisi za Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa –Alhananah-.
  • 2- Maonyesho ya vitabu ya Atabatu Abbasiyya katika mji wa Najafu Ashrafu, barabara ya Rasuul (s.a.w.w) karibu na ofisi ya Shekhe Fayaadh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: