Ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) usiku wa Ijumaa, umeshuhudia usomwaji wa Dua Komaili kwa ushiriki wa kundi kubwa la waumini.
Ibada ya kusoma dua, imefanyika katika mazingira tulivu kwa Baraka za mnasibishwaji wa Dua na ushiriki wa idadi kubwa ya mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Watumisi wa Atabatu Abbasiyya tukufu huandaa mazingira mazuri ya usomaji wa dua, huweka vitabu vya dua na kuandaa sehemu maalium kwa ajili ya ibada hiyo.























