Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wameweka mapambo meusi ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na maombolezo ya kifo Ummul-Banina (a.s).
Wameweka mabango kwenye pambo (sega) linaloangalia ukumbi mtukufu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na maeneo yanayozunguka sehemu hiyo kwa kutumia vifaa maalum.
Ataba tukufu imeandaa sehemu rasmi kwa ajili ya kuomboleza msiba huo, ili iweze kutoa huduma bora kwa mazuwaru watukufu.





