Maukibu ya watu wa Balad inaomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s)

Maukibu ya watu wa Balad imeomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Muimbaji Husseini Haidari Baldawi amesema “Watu wa Balad wameomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) katika Atabatu Abbasiyya sambamba na kutoa pole kwa mbeba bendera ya Imamu Hussein Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Maukibu ya watu wa Balad na kikundi cha Imamu Hussein (a.s), wamezowea kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) mbele ya kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) na huandika haja za waumini baada ya kumaliza majlisi ya uombolezaji”.

Akasema kuwa “Tunaishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ushirikiano wake katika kufanya maombolezo, sambamba na msaada endelevu kwa vikundi vya maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika kuadhimisha matukio ya kidini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: