Atabatu Abbasiyya inakumbuka historia ya Ummul-Banina (a.s) na msimamo wake.

Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia majlisi za kuomboleza, inakumbuka kifo cha Ummul-Banina (a.s) mbele ya watumishi wengi wa Ataba tukufu na mazuwaru.

Mhadhiri wa Majlisi Sayyid Akram Batwat amesema “Tumefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s), historia yake tukufu, na msimamo wake katika kunusuru familia ya Mtume (s.a.w.w)”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya huwasiliana na waumini kupitia majlisi tukufu, sambamba na kuhimiza harakati mbalimbali kama kuandika kitabu cha historia ya Ummul-Banina (a.s) na kuangalia baadhi ya mapendekezo ya kielimu yanayotolewa na Ataba tukufu”.

Akabainisha kuwa “Majlisi zinamchango mkubwa wa kujenga mazingira ya kiroho kwa jamii na kuwalinda waumini na fikra potofu”.

Atabatu Abbasiyya tukufu hutoa umuhimu wa pekee katika kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s), kwa lengo la kubeba ujumbe wao (a.s) na kufuata mwenendo wao mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: