Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s).
Ratiba za majlisi zinazofanywa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) za kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) zitadumu kwa siku tatu.
Kitengo kinafanya majlisi za kuomboleza ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala, kwa lengo la kuangazia historia ya Ummul-Banina (a.s) na kueleza umuhimu wa kufanya kumbukizi za Ahlulbait (a.s).



