Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amewataka wabobezi wa lugha ya kiarabu kuvutia watu kwenye lugha hiyo na kuonyesha uzuri wake.
Amesema hayo alipokutana na ujumbe wa jumuiya ya Al-Ameed pembezoni mwa nadwa ya kielimu inayosimamiwa na jumuiya hiyo katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya lugha ya kiarabu, akasikiliza maelezo kuhusu kazi za jumuiya na harakati za kueneza lugha ya kiarabu katika jamii mbalimbali.
Muheshimiwa akasisitiza umuhimu wa kuonyesha uzuri wa lugha ya kiarabu, akasema kuwa Qur’ani tukufu imetunzwa kwa lugha fasaha ya kiarabu na imeonyesha uzuri wa lugha hiyo.
Akatoa wito kwa wabobezi wa lugha ya kiarabu kuvutia watu kwenye lugha hiyo kupitia harakati mbalimbali sambamba na kuonyesha uzuri wa lugha ya kiarabu.
Rais wa kitengo cha harakati katika jumuiya ya Al-Ameed, Dokta Ali Kadhim Maslawi amesema, pembezoni mwa hafla ya siku ya kimataifa ya lugha ya kiarabu, jumuiya imefanya nadwa maalum yenye anuani isemayo: (Lugha ya kiarabu katika macho ya watazamaji wake) na pembezoni mwa nadwa hiyo tukapata nafasi ya kukutana na Muheshimiwa Sayyid Swafi.
Akaongeza kuwa, Tumeongea kuhusu umuhimu wa lugha ya kiarabu na dharura ya kuifundisha katika maeneo ya kitamaduni na kielmu, sambamba na kuitumia kwa usahihi ikiwemo kufanya mashindano ya mashairi na nadwa mbalimbali.