Rais wa kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Khaliil Mahadi Hanun amesema “Atabatu Abbasiyya imepokea watumishi wa Atabatu Husseiniyya waliokuja kutoa pole kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina (a.s), wakafanya majlisi ya kuomboleza iliyohudhuriwa na watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na kundi kubwa la mazuwaru, zikasomwa qaswida na tenzi za kuomboleza zilizoamsha hisia za huzuni na majonzi katika nyoyo za waumini”.
Mshauri wa katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Fadhili Auzi amesema “Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimeshuhudia mawakibu za kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) na watumishi wa Atabatu Husseiniyya wametoa pole kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huo”.
Watumishi wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala, hufanya maukibu ya pamoja kwenye matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) katika kipindi chote cha mwaka.
































