Majmaa-Ilmi imeomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) katika mji wa Karbala

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s).

Imefanya hivyo kupitia majlisi ya kuomboleza iliyoratibiwa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa katika mji wa Karbala.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ali Maitham, ikafuatiwa na muhadhara kutoka kwa Shekhe Muntadhiru Shimri, aliyebainisha utukufu wa Ummul-Banina (a.s) na namna alivyojitolea.

Muhadhara ukafuatiwa na qaswida ya kuomboleza kutoka kwa Sayyid Jawadi Halo iliyo eleza kuhusu msiba huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: