Muhadhara wa kidini umetaja misimamo ya Ummul-Banina (a.s)

Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa muhadhara wa kidini katika kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s), ulioeleza nafasi yake katika kushikamana na mafundisho ya Mtume (s.a.w.w).

Mhadhiri wa majlisi Sayyid Akram Batwat amesema “Muhadhara umetolewa ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya, kwa lengo la kueleza historia ya Ummul-Banina (a.s) na msimamo wake katika kuwanusuru Ahlulbait (a.s), hakika alikuwa mfano hai katika kutekeleza mafundisho ya Mtume (s.a.w.w) anaefaa kuigwa maishani”.

Akasema kuwa “Kuhuisha matukio ya kidini husaidia katika kujenga roho kwa wanajamii sambamba na kuimarisha uwezo wa kufikiri na kupambana na changamoto”.

Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya majlisi zinazohusu matukio ya Dini na Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kufikisha ujumbe na kueleza mwenendo wao mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: