Kongamano litafanywa chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu tarehe (19 – 20/12/2024m) katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani ya Ataba tukufu.
Siku ya kwanza: kongamano litaanza saa saba na nusu mchana, ambapo mada nne zitawasilishwa.
Siku ya pili: litaanza saa tatu asubuhi, ambapo kutakua na maonyesho ya nasaha za Marjaa-Dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Sistani kwa vijana sambamba na kuangazia namna ya kunufaika na nasaha hizo.
Mada kuu za kongamano ni:
- 1- Habari na mitandao ya mawasiliano ya kijamii.
- 2- Mtazamo wa kijamii kwa Marjaiyya.
- 3- Utambulisho wa jamii.
- 4- Misingi ya maarifa na utamaduni.