Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha ratiba ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s).
Ratiba imedumu kwa siku mbili na ilikuwa na vipengele vingi, kikiwemo kipengele cha igizo lenye anuani isemayo (Tasbihatu-Ithaar) lililo onyesha kujitolea kwa Ummul-Banina (a.s) na usia aliotoa kwa watoto wake, wasimame imara pamoja na Imamu Hussein (a.s), muhadhara wa kielimu wenye anuani isemayo (Umaalum na utukufu wa surat Faatihah), umeangazia maana za ndani katika sura hiyo na kubainisha baadhi ya utukufu wake na ujumbe uliopo kwenye sura hiyo.
Ratiba imepambwa na ugawaji wa chakula cha Ummul-Banina (a.s), usomaji wa Qaswida na tenzi na kutoa pole kwa Imamu wa zama (a.f) kutokana na msiba huo.




