Mashamba ya Atabatu Abbasiyya yanachangia soko la ndani kwa aina tofauti za tende

Shirika la uchimi Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya linachangia soko la ndani kwa kuingiza aina tofauti za tende.

Msaidizi wa kiongozi mkuu wa idara ya kilimo na mazao ya wanyama, Mhandisi Ali Maz-ali Laaidh amesema “Tende zimepandwa kwenye shamba lenye ukubwa wa dunam 1500 katika mashamba ya Khairaatu Abulfadhil Abbasi (a.s), tende hizo ni za asili na zinaubora wa hali ya juu”.

Akaongeza kuwa “Umwagiliaji unafanywa kwa kutumia mahodhi na visima, pamoja na mtandao wa umwagiliaji unaochukua eneo la dunam 68 na 80 kwenye maeneo tofauti”.

Akafafanua kuwa “Msimu wa kilimo huanza kwa kupanda miche ya mitende katika mwezi Novemba na mavuno hufanywa mwishoni mwa mwezi wa April”.

Akasema “Kuna vitu vingi vinavyosaidia kuzalisha tende bora, kwa mfano uchaguzi wa mbegu nzuri, uandaaji wa shamba, uwekaji wa viatilifu na utumiaji wa mitambo ya kisasa”.

Akasisitiza kuwa “Wasimamizi wa mradi wanauzowefu mkubwa kutokana na kusimamia miradi mingi ya kilimo inayofanywa na Atabatu Abbasiyya, jambo linalosaidia kuwa na mafanikio makubwa ya kuzalisha mazao bora”.

Atabatu Abbasiyya inaingiza sokoni mazao kutoka kwenye shamba lenye ukubwa wa dunam elfu 19, ambapo huvunwa mazao toafauti yenye ubora mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: