Kitengo cha habari na utamaduni: Maahadi ya turathi za mitume imepokea zaidi ya wanafunzi elfu 3 kutoka nchi 22

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimesajili zaidi ya wanafunzi elfu 3000 kutoka nchi 22, watakaosoma katika Maahadi ya turathi za mitume masomo ya hauza kwa njia ya mtandao yanayofundishwa kwa lugha ya kiarabu na kiurdu, katika mwaka wa masomo 1445h.

Mkuu wa Maahadi Shekhe Hussein Turabi amesema “Maahadi imepata muitikio mkubwa mwaka huu, wanafunzi wengi wamejiandikisha masomo kwa njia ya mtandao, jumla ya wanafunzi elfu 3 walijiandikisha, jambo hilo limeifanya Maahadi kuwa kinara katika sekta ya elimu”.

Akaongeza kuwa “Raia wa Iraq waliojisajili walifika 1333, Pakistani 1501, India 110 na wanafunzi kutoka nchi zingine kama Afghanistani Iran, Marekani, Kenya na Lebanon, hakika wanafunzi wanatoka mataifa mbalimbali yenye tamatuni tofauti”.

Mafanikio hayo ni makubwa kwa Maahadi katika usambazaji wa elimu ya Ahlulbait (a.s) kwa kutumia mitandao ya kisasa, aidha inachangia kuunganisha wanafunzi katika elimu ya dini kutoka mataifa tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: