Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wameweka mapambo yanayoashiria furaha katika kuadhimisha mazazi ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).
Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Abidina Quraishi amesema “Wtumishi wa kitengo wameweka mapambo yanayoashiria furaha, ambayo ni mauwa na mabango, katika mnasaba wa kuadhimisha mazazi ya Mbora wa wanawake wa ulimwenguni Bibi Fatuma Zaharaa (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Kazi hiyo imehusisha ujengaji wa jukwaa mbele ya mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba kuandaa majukwaa yaliyopo katika ukanda wa kijani kibichi, vitalu vya Alkafeel na maeneo mengine yaliyochini ya Atabatu Abbasiyya”.
Kwa mujibu wa maelezo ya makamo rais wa kitengo hicho amesema, kutakuwa na hafla itakayofanywa na Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel ndani ya mji mkongwe na kwenye barabara zinazoelekea Ataba tukufu, itahusisha ugawaji wa halwa, mauwa na marashi kwa mazuwaru watukufu.








