Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza majina ya washindi wa shindano maalum la kuadhimisha mazazi ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).
Sharti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa ahudhurie hafla ya kuadhimisha mazazi ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) itakayofanywa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Jumamosi (21/12/2024) sawa na mwezi (19 Jamadal-Aakhar 1446) baada ya swala ya Magharibi na Isha.
Iwapo mshindi atapata udhuru wa kushindwa kufika kwenye hafla hiyo, atalazimika kwenda katika ofisi za wahasibu wa Ataba tukufu ndani ya muda usiozidi siku nne toka kutangazwa kwa matokeo haya, akiwa na nyaraka zinazomthibitisha (kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria).

