Mkuu wa kitengo Hasanaini Mussawi amesema “Watumishi wa kitengo wameandaa hafla ya kuadhimisha mazazi ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kupitia mkakati wa kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Hafla imejumuisha vipengele tofauti, ukiwemo muhadhara kuhusu historia ya Bibi Zaharaa (a.s) uliotolewa na Shekhe Zamaan Alhasanawi, qaswida kuhusu mbora wa wanawake wa ulimwenguni (a.s) kutoka kwa Muhammad Fatwimi”.
Akasema “Chuo hufanya hafla hizi kutokana na umuhimu wake katika kuimarisha misingi ya malezi na elimu baina ya wanafunzi na watumishi”.









