Majlisi imehudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Ashqar, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami na baadhi ya viongozi wa Ataba na mazuwaru.
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya majlisi katika Ataba tukufu Dokta Mushtaqu Ali amesema “Majlisi ni sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na umezungumzwa utukufu wa mwanamke bora wa ulimwenguni (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Hafla imehudhuriwa na taasisi za Qur’ani kutoka ndani na nje ya Karbala, sambamba na ushiriki wa wasomaji wa Ataba tukufu, ikahitimishwa kwa kugawa zawadi za washindi wa shindano la kimtandao lililofanywa kufuatia mnasaba wa tukio hili”.















