Kitengo cha Dini kinaadhimisha mazazi ya Bibi Zaharaa (a.s)

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimeadhimisha mazazi ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Rais wa kitengo Shekhe Swalahu Karbalai amesema “Kitengo kimeandaa muhadhara wa kidini ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha mazazi ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), uliojikita katika kueleza historia yake takatifu na utukufu wake katika uislamu”.

Akaongeza kuwa “Matukio haya matukufu huwajenga waumini kiroho na kuwafungamanisha na Ahlulbait (a.s)”.

Akasema kuwa “Wafuasi wa Ahlulbait (a.s) hujali sana matukio ya kihistoria hususan yanayowaunganisha na Ahlulbait (a.s)”.

Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya majlisi za kidini katika kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kuhuisha utajo wao na kueleza utukufu wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: