Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake inaadhimisha mazazi ya Bibi Zaharaa (a.s)

Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imeadhimisha mazazi ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Kiongozi wa Maahadi Bibi Manaar Aljaburi amesema “Maadhimisho yamefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ukafuata muhadhara wa kidini wenye anuani isemayo (Zaharaa ni kigezo changu), kukawa na kipengele cha maswali na majibu kwa washiriki”.

Akaongeza “Hafla imeshuhudia usomaji wa Qur’ani kwa kikundi kutoka kwa kikosi cha Fedha na qaswida za kidini zilizoeleza utukufu wa Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kutoka kwenye kikosi cha Swidiqah”.

Akafafanua kuwa “Maahadi imetoa zawadi kwa wanafunzi wenye majina ya Bibi Zaharaa (a.s)”, akasema “Hafla ilihitimishwa kwa qaswida za kuwasifu wajukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: