Kiongozi wa idara ya habari za Qur’ani katika Maahadi Sayyid Imaad Mankushi amesema “Maahadi imeomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) katika Majmaa Alqami chini ya Ataba tukufu, kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi 80 katika wilaya ya Husseiniyya mkoani Karbala”.
Akafafanua kuwa “Hafla imepambwa na mhadhara wa kidini ulioeleza historia ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na utukufu wake, kisha zikasomwa tenzi na qaswida”.
Akabainisha kuwa “Maahadi inalenga kujenga misingi ya kimaadili na kidini kwa wanafunzi, ili kupambana na fikra potofu zinazopandikizwa katika jamii”.














