Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefanya warsha ya kutambulisha mlango wa Iraq katika chuo kikuu cha Karkha.
Kiongozi wa idara ya kudhibiti maudhui katika kituo cha faharasi chini ya kitengo Sayyid Ali Twalib amesema “Tumefanya warsha ya kutambulisha mlango wa Iraq kwa watumishi wa chuo kikuu cha Karkha, tumeeleza umuhimu wa mlango huo na jinsi watafiti wanavyo nufaika nao katika kufikia vyanzo vya kielimu vilivyopo kwenye mlango huo”.
Akaongeza kuwa “Warsha imejikita katika kufafanua namna ya kutumia mlango, akasema kuwa unategemea (sehemu la laam), ambayo imeingizwa maktaba na makumbusho kwenye jukwaa moja katika intanet”.
Akaendelea kusema “Warsha imetoa maazimio muhimu, miongoni mwake ni umuhimu wa kuingiza jukwaa hilo katika mitandao ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, ili wanafunzi waweze kunufaika nayo kama chanzo madhubuti cha taaluma”.

