Sayyid Swafi amezindua kitabu cha swala kilichoandikwa na Allamah Abu Hassan Almashkini

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amezindua kitabu cha swala kilichoandikwa na Allamah Abu Hassan Almashkini.

Uzinduzi huo umefanywa katika nadwa ya kielimu iliyopewa jina la (Mirza Abu Hassan Almashkini na urithi wake wa kifiqhi, kitabu cha swala kama mfano), iliyofanywa mbele ya wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya na walimu wa hauza katika mkoa wa Najafu.

Uchapishwaji wa kitabu hicho chenye juzuu kumi, umesimamiwa na kituo cha kuhuisha turathi, kitabu kinamfumo mzuri jambo ambalo linakifanya kuwa marejeo makuu kwa wasomaji na watafiti, kitabu hicho kimehakikiwa na kituo cha Shekhe Tusi.

Kitabu kimehakikiwa kupitia nakala mbili, nakala iliyotolewa na muandishi mwenyewe na nakala iliyotolewa na mwanafunzi wake Sayyid Murtadha Khalkhali, Sayyid aliandika aliyotoa kwa mwalimu wake, akasahihisha baadhi ya maeneo na kufafanua baadhi ya sehemu zingine.

Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya kazi kubwa ya kulinda turathi za kielimu za wanachuoni watukufu, na kuhakikisha zinafika katika vizazi vijavyo zikiwa katika muonekano bora, sambamba na kufanya miradi ya kielimu inayoendelea kubakiza heshima ya hauza na kuifanya kuwa kinara katika elimu na maarifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: