Kitengo cha uboreshaji kinatoa muhadhara kuhusu Nahajul-Balagha kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kinatoa muhadhara wa kusherehesha madhumuni ya Nahajul-Balagha kwa watumishi wa Ataba tukufu.

Mhadhiri Shekhe Hani Rabii amesema “Atabatu Abbasiyya inafanya mradi mkubwa wa kuhifadhi Nahajul-Balagha na Fiqhi, kwa lengo la kusambaza elimu ya kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), kwa kuwahifadhisha watumishi maana za khutuba za Nahajul-Balagha na ujumbe wake”.

Akaongeza kuwa “Huu ni mwaka wa tatu toka ianzishwe ratiba ya kuhifadhisha watumishi wa Ataba tukufu khutuba za Nahajul-Balagha chini ya mfumo maalum”.

Mmoja wa watumishi wa kitengo, Sayyid Muntadhiru Hassan amesema “Ratiba ya Nahajul-Balagha inasimamiwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, imeanza zaidi ya miaka miwili iliyopita na bado inaendelea”.

Akabainisha kuwa “Muhadhara hutolewa kila siku ya Alkhamisi kwa muda wa saa mbili, mbele ya washiriki 15 miongoni mwa watumishi”, akasema kuwa “Ratiba inalenga kuongeza idadi ya watu wanaohifadhi kitabu cha Nahajul-Balagha na kujenga uwelewa wa kitamaduni kwa watumishi wa Ataba tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: