Hafla inafanywa na Jumuiya ya Skaut chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo (Vizazi katika mwenendo wa Mitume) tarehe 27 – 28/12/2024m.
Hafla imehudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu Sayyid Liith Mussawi na baadhi ya wakuu wa vitengo bila kusahau wageni waalikwa na wazazi wa washiriki.
Wanachama wa Skaut zaidi ya 1000 wameshiriki kwenye hafla hiyo, wametumia mlango wa Imamu Ali na Imamu Hussein (a.s) na kukusanyika katika Sardabu ya Maimamu hao wawili (a.s), wakati wakijiandaa kuingia kwenye ukumbi wa Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kufanya tukio la Skaut katika haram hiyo takatifu.
Hafla inahusisha mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kula kuapo cha Skaut, kusoma ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya haram tukufu, kufanya maonyesho ya Skaut katika uwanja wa michezo wa kimataifa uliopo Karbala, kutembelea miradi inayofanywa na jumuiya ya Skaut hapa Iraq katika barabara ya Ataba tukufu pamoja na mambo mengine.




























