Kuhitimisha kongamano la kielimu Ruhu-Nubuwwah awamu ya saba

Idara ya shule za Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya, imehitimisha ratiba ya kongamano la kitamaduni Ruhu-Nubuwwah awamu ya saba.

Kiongozi wa idara Bibi Bushra Kinani amesema “Idara ya shule za Alkafeel imehitimisha kongamano la kielimu Ruhu-Nubuwwah awamu ya saba, katika mnasaba wa kuadhimisha mazazi ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na kuangazia fikra zake kwa kujadili tafiti za kielimu”.

Kuhitimisha ratiba ya kongamano la kielimu Ruhu-Nubuwwah awamu ya saba

Idara ya shule za Alkafeel tawi la wasichana katika Atabatu Abbasiyya, imefanya kongamano la kielimu Ruhu-Nubuwwah awamu ya saba.

Kiongozi wa idara Bibi Bushra Kinani amesema “Idara ya shule za Alkafeel imehitimisha kongamano la kielimu Ruhu-Nubuwwah awamu ya saba, katika mnasaba wa kuadhimisha mazazi ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s), na kuangazia fikra na athari yake (a.s), kufatia kujadili tafiti za kielimu”.

Akaongeza kuwa “Akatangazwa Dokta Muhammad Aribi kuwa mshindi wa pili kutokana na utafiti wake uitwao (Kujitolea kwa Bibi Zaharaa (a.s) na msingi wa vitendo baina ya nafsi na akili –surat Insaan kama mfano-, na mtafiti Ummul-Banina Yusufu Jamali kutoka Baharain akawa mshindi wa tatu, kutokana na tafiti yake aliyofanya kwa lugha ya kiengereza isemayo (Nafasi ya Bibi Zaharaa (a.s) kama mfano katika kuimarisha utambulisho na heshima kwa wanawake wa Baharaini), hakupatikana mshindi wa kwanza kwa sababu tafiti zote hazikufikia viwango vinavyo takiwa kwa mshindi wa kwanza”.

Bibi Kinani amemshukuru kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na watumishi wa Atabatu Abbasiyya kwa kazi kubwa waliyofanya ya kuandaa kongamano hili.

Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kongamano la Ruhu Nubuwwah, imekuwa ikihuisha turathi za Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: