Kitengo cha maarifa kimechapisha toleo la nne la kitabu cha (Midhmaar Turathi)

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimechapisha juzuu la nne la kitabu cha (Midhmaar turathi).

Uchapishwaji wa kitabu hicho umesimamiwa na idara ya habari za maarifa chini ya kitengo, kwa lengo la kutunza maswali ya mashindano ya maarifa ya turathi katika mwezi wa Ramadhani na kuongeza unufaikaji wake.

Kitabu kinamaswali 450 yanayohusu sekta mbalimbali za turathi za kiislamu na miji ya Iraq, maswali yamelenga elimu ya sekula na turathi, kina milango kumi, sambamba na kuandika majibu sahihi ya kila swali.

Msimu wa tano wa mashindano utajikita katika maarifa ya turathi na picha, kwa kiasi ambacho itakua na mvuto wa pekee katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: