Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza kuanza kwa mashindano maalum kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s).
Majina ya washindi kumi wa mwanzo yatatangazwa jioni ya Jumanne (31/12/2024) kwenye jukwaa la Atabatu Abbasiyya tukufu, sharti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s) itakayofanywa kwenye uwanja wa mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) (1/1/2025) siku ya Jumatano.
Iwapo mshindi atapata udhuru wa kushindwa kufika kwenye hafla hiyo, atatakiwa kwenda katika kitengo cha wahasibu wa Atabatu Abbasiyya ndani ya muda usiozidi siku nne (4) toka kutangazwa kwa matokeo, akiwa na nyaraka zinazo mthibitisha (kitambulisho cha uraia au hati ya kusafiria).
