Idara ya wahadhiri wa Huseiniyya tawi la wanawake imeandaa ratiba ya Maraqil-Ula katika mji wa Karbala

Idara ya wahadhiri tawi la wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya (Maraqil-Ula) kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za mkoa wa Karbala.

Kiongozi wa idara Bibi Taghrida Tamimi amesema “Awamu mpya ya ratiba ya (Maraqil-Ula) katika mwaka huu wa masomo, inafanywa kwa msaada wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi na maelekezo yake, ratiba inahusisha wanafunzi 150 kutoka shule ya Alhuriyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala”.

Akaongeza kuwa “Ratiba inavipengele vya kitamaduni, kielimu, kuwajengea uwezo katika mambo mbalimbali, maigizo, kwa lengo la kuwapa fikra muhimu zitakazo wafanya kuwa watu wazuri katika jamii”.

Idara hufanya shughuli mbalimbali na kutoa mihadhara tofauti kwa lengo la kujenga misingi ya kitamaduni na kidini katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: