Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimechapisha kitabu kipya kwa anuani ya (Masaailu Fiqihiyyah Istidilaliyyah).
Uhakiki na uchapaji wa kitabu hicho umefanywa na idara ya wahakiki chini ya kituo cha turathi za Karbala, nacho ni katika uandishi wa Sayyid Mirza Muhammad bun Mirza Radhwawi Mash-hadiyyu, mmoja wa wanachuoni wakubwa wa Imamiyya karne ya kumi na tatu hijiriyya.
Kitabu kinajuzuu mbili, juzuu ya kwanza inakurasa (375) na juzuu ya pili inakurasa (461), jumla ya mambo (218) ya kifiqhi yameandikwa, miongoni mwa mambo hayo ni, hukumu za twahara za maji na udongo, mambo tofauti ya kifiqhi yameandikwa pamoja na shuhuda zake sambamba na kutaja maoni ya wanachuoni wa sasa na wazamani.
Kituo cha turathi za Karbala hufanya uhakiki wa vitabu muhimu na kuvichapisha sambamba na kuhuisha turathi za Karbala.