Atabatu Abbasiyya imewekwa mapambo yanayo ashiria furaha kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Baaqir na Haadi (a.s)

Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wameweka mapambo yanayoashiria furaha kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s).

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Watumishi wa kitengo wameweka mauwa na mabango yanayo ashiria furaha kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Kazi ya kushona vitambaa na kuandaa mabango imesimamiwa na idara ya usonaji, chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya, mabango yamewekwa kwenye milango na sehemu mbalimbali za Ataba tukufu”.

Akasema kuwa “Lengo la kuhuisha matukio haya ni kusambaza elimu ya Ahlulbait (a.s) na kuheshimu mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ya kushikamana na kizazi chake kitakatifu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: