Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea na mradi wa ujenzi wa ghala za Ataba tukufu katika barabara ya (Najafu – Karbala).
Mhandisi mkazi wa mradi Sayyid Muhammad Jafari amesema “Kazi ya ujenzi wa ghala za Ataba tukufu inaendelea, huu ni mradi wa 8 wenye ghala 6 zitakazokuwa na majukumu tofauti”.
Akaongeza kuwa “Kazi ya ujenzi katika mradi wa 8 inaendelea, nayo inafungamanishwa na mradi wa 2 kwa kutumia nguvu ya jua”.
Akabainisha kuwa “Ujenji wa boma umekidhi viwango vinavyohitajika, kiwango cha ukamilifi ni %65, zimebaki hatua chache kukamilisha uradi huo na kufanya ufunguzi”.
Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya miradi tofauti ya ujenzi, ili kusaidia sekta ya uzalishaji na kukidhi mahitaji ya wananchi kwa kutoa huduma mbalimbali.









