Chuo kikuu cha Al-Ameed kimefanya nadwa ya kutambulisha maktaba yake kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa udaktari wa meno

Chuo kikuu cha Al-Ameed kimefanya nadwa ya kutambulisha maktaba yake kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika kitivo cha udaktari wa meno, kwa lengo la kuwatambulisha huduma zinazotolewa.

Nadwa imejikita katika kueleza namna ya kunufaika na huduma zinazotolewa na maktaba kwa walimu na wanafunzi.

Imeangazia umuhimu wa kusoma na kujifunza katika kuongeza maarifa na uwezo wa fikra, sambamba na kujadili namna ya kuifanya maktaba kuwa uwanja wa masomo na kupata uzowefu.

Ratiba hiyo ni sehemu ya juhudi za chuo kikuu cha Al-Ameed za kukuza utamaduni wa kusoma, kufanya tafiti za kielimu na kusaidia wanafunzi katika safari yao ya kutafuta elimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: