Kitengo cha habari na utamaduni kimechapisha kitabu kuhusu fikra za Imamu Muhammad Albaaqir (a.s)

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimechapisha kitabu chenye anuani isemayo (Imamu Muhammad Albaaqir –a.s- ni mwangaza katika fikra na lugha).

Uchapishaji wa kitabu umesimamiwa na kituo cha tafiti Al-Ameed, nalo ni chapisho la ishirini na tatu katika mfululizo wa kitabu cha Al-Ameed, chapisho hilo limetolewa sanjari na maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Albaaqir (a.s), kwa lengo la kuangalia mchango wake katika elimu ya Uislamu.

Kitabu kimeandika tafiti za kielimu kutokana na mambo yaliyoshuhudiwa katika zama za Imamu (a.s), sambamba na kueleza changamoto za kifikra na kisiasa zilizokuwepo wakati huo, ikiwemo kusambaa kwa fikra potofu, mikakati ya utawala wa Umawiyya na mpasuko wa jamii.

Kitabu kimeandika kazi kubwa ya kupatanisha (islahi) aliyofanya Imamu Albaaqir (a.s) pamoja na kurekebisha fikra potofu na mafundisho ya Dini katika zama hizo, urithi wake utaendelea kuwa msingi wa kuigwa katika umma wa kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: