Kitengo cha kusimamia haram kimekamilisha maandalizi ya kuadhimisha watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Rajabu

Kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya kimekamilisha maandalizi ya kuadhimisha Maimamu wa Ahlulbait (a.s) waliozaliwa katika mwezi wa Rajabu.

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Watumishi wa kitengo wamekamilisha maandalizi ya kupokea mazuwaru watakaokuja kuadhimisha mazazi ya Ahlulbait (a.s), mambo yote ya lazima tayali wamesha andaliwa sambamba na kuweka muongozo wa utembeaji ndani ya Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Maandalizi yamehusisha kuandaa sehemu ya kufanyia hafla za maadhimisho ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya, ikiwa ni pamoja na hafla kubwa itakayofanywa kwenye uwanja wa mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akafafanua kuwa “Hafla ya kwanza itakayofanywa katika mwezi huu ni maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s), Ataba tukufu imepambwa vizuri pamoja na barabara zinazoelekea kwenye Ataba zimeweka mauwa kufuatia maadhimisho hayo matakatifu”.

Atabatu Abbasiyya tukufu huadhimisha matukio yakidini yanayohusu kumbukumbu za Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: