Atabatu Abbasiyya tukufu, imewapa zawadi washindi wa shindano maalum la kuadhimisha mazazi ya Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s).
Tukio hilo ni katika vipengele vya hafla iliyofanywa na Atabatu Abbasiyya katika uwanja wa mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Washiriki wa shindano hilo walifika (2271), majibu sahihi yalikua (196), ambapo ililazimika wachaguliwe washindi (10) kwa njia ya kupiga kura, wakakabidhiwa zawadi zao na rais wa kitengo cha Dini katika Ataba tukufu Shekhe Swalahu Khafaji.
Washindi walioshindwa kufika katika hafla hiyo, wanatakiwa waende katika ofisi za wahasibu wa Atabatu Abbasiyya kuchukua zawadi zao ndani ya siku nne toka kutolewa kwa tangazo hili, wakiwa na nyaraka zinazo wathibitisha (kadi ya uraia au hati ya kusafiria).